Naam pasi na shaka u mzima na unaendelea vyema kiafya, karibu tena kwenye taarifa fupi na mimi muwasilishaji wako NPV nikiripoti moja kwa moja kutokea hapa Bangladesh.

Mwaka 2004 wakati sheikh, Amir Junaid Muhadith ‘Loon’ anatemana na Bad Boys Records ya mtu mzima P.Diddy na kuanzisha Record Label yake ya Boss Up Entertainment inatajwa kuwa moja kati ya changamoto kubwa alizokuwa akizipitia kabla ya kuamua kuachana kabisa na habari za muziki na kuingia kwenye dini ilikuwa ni fatwa fatwa/daiwa daiwa ya fedha ambazo kimsingi zilikuwa kwenye makubaliano ya kimikataba na Bad Boys Records. Diddy alikuwa na utaratibu wa kuwatimbia popote pale watakapoenda kufanya kazi zao za kimuziki wasanii ambao waliotoka kwenye Label yake bila kumalizana nao, Loon hakuwahi kulizungumzia hili kwa upana lakini moja ya sababu kubwa zinazotajwa kumfanya yeye aachane na muziki mbali na dini ni madeni ya kimkataba aliyokuwa akidaiwa na Bad Boy Records chini ya Diddy baada ya kuacha kufanya kazi na Label hiyo ingawa yeye na Diddy bado walikuwa ni marafiki wa karibu kabisa, ilikuwa ukitoka Bad Boy Records na ukaenda kufanya mitikasi yako mengine Diddy alikuwa hana time kabisa na wewe lakini ukianza tu kuimba, Diddy huyu hapa anataka chake yale yale ya kimkataba kama ya Banky W na Wizkid.

Wapo wasanii wa Bad Boy Records ambao walikuwa hawaridhishwi na usimamizi na mikataba ya Records Label hiyo lakini wengi hawakuwahi kusema pindi wakiwa ndani kiasi cha kupelekea wengine kuacha kabisa muziki baada ya kutoka kwenye Label hiyo kuepuka fatwa fatwa ya Diddy pindi ukifanya muziki nje ya Bad Boy wakati mkiwa bado hamjamalizana. Wapo wasanii wengine ambao walizipamba na kuzisifu sana records label zao mpya ambazo waliingia kufanya nazo kazi mara baada ya kutemana na Bad Boy Records ambapo napo walipasifu kabla pindi wakiwa ndani.

“Ilikuwa ni ndoto yangu kufanya kazi chini ya Record label hii kubwa duniani, naamini nitakuwa mkubwa zaidi na kuacha historia kwa mafanikio makubwa tofauti na kule nilipotoka” – Mmoja wa wasanii baada ya kutoka Bad Boy Records.

Unadhani ni kweli records label hizo mpya walizokuwa wanaingia nazo makubaliano zilikuwa zinaupiga mwingi kama walivyozipamba au ganzi ya kutosikia maumivu (kusema ya mayoni pindi wakiwa Bad Boys Records) ilikuwa imeisha?tujiunge na ripota wetu Mgenge kutoka ZeTrend ya Plus TV channel namba 294 kwenye king’amuzi cha DStv, Jumatatu hadi Ijumaa 12:30 za jioni kwa taarifa kamili.

Moja kati ya vitu ambavyo vilimpa wakati mgumu Sir Alex Ferguson wakati akiwa Manchester United ni kuwanyoosha wachezaji wake kitabia ambapo kiuhalisia ukizungumzia makocha ambao waliishi na wachezaji wenye vichwa vigumu na watukutu duniani nafikiri Ferguson ni mmoja wapo. Mmoja kati ya wachezaji ambao walimsumbua sana na kumpa wakati mgumu Ferguson ni Mtoto wa kiingereza Wayne Rooney ambaye alipendwa sana na kocha huyo kwasababu ya kipaji chake kikubwa, uwezo mzuri lakini alikuwa na tabia ambazo zilimkwaza sana Ferguson na mara zote alikuwa akijaribu kumshape vile alivyotaka yeye, ukisoma kwenye kitabu cha My Autobiography cha Mzee Fergie kwenye sura ya 24 ukurasa wa 151 amemuelezea vizuri kijana wake huyu.

Rooney anaamini katika vipindi vigumu na vibaya ambavyo amepitia kwenye uchezaji wake wa soka basi ni ndani ya Manchester United akiwa chini ya Sir Alex Ferguson, mwaka 2010 Manchester City walihusishwa kumuhitaji Wayne Rooney na waliweka ofa ya mshahara mkubwa mezani ili wamnase nyota huyo lakini United hawakuwa tayari kutoa kiasi hiko cha fedha kumlipa Rooney kama mshahara. Ferguson alikuwa bado anamuhitaji Rooney kwenye kikosi chake kwani bado alikuwa kwenye mipango yake, kutokana na tabia za Rooney aliona akiishawishi bodi impe Rooney fedha hizo nyingi kama mshahara ili asaini mkataba mpya basi baadae Rooney atamdharau yeye kutokana na fedha, Fergie alienda kwenye bodi ya United akawaambia mpeni Rooney anachotaka ili asaini mkataba mpya kwani bado tunamuhitaji lakini hakikisheni mshahara wangu mnauongeza maradufu kumzidi yeye kwenye huu mkataba wake mpya, bodi ilifanya kama Mzee Fergie alivyoagiza na Rooney akasalia klabuni. Baada ya miaka 9 ya Wayne Rooney klabuni, Mzee Ferguson anastaafu rasmi kufundisha soka na wanaingia makocha wengine ndani ya United ikiwemo Mdachi Luis Van Gaal ambaye aliingia United mwaka 2014 kabla ya kutimuliwa mwaka 2016.

Wayne Rooney akiwa anakaribia kustaafu soka alifanya mazungumzo na chombo kimoja cha habari ambapo kwenye mazungumzo hayo aliulizwa yupi ni kocha bora kwa upande wake na bila kusita Wayne Rooney alisema Louis Van Gaal ni kocha bora kwa 100% kati ya makocha wote aliowahi kufanya nao kazi ikiwemo Sir Alex Ferguson ambapo Rooney hakuishia hapo alimpamba Van Gaal kwa kusema kuwa ni kocha mwenye mbinu bora, mtulivu na mwenye kujali wachezaji wake tofauti na Ferguson ambaye anatajwa kuwa dikteta na mkali kwa wachezaji wake jambo ambalo hata nyota wa zamani wa klabu hiyo Roy Keane aliwahi kulisema huku akiwapamba zaidi makocha wengine na kumsagia kunguni Ferguson ambaye alikuwa Mwalimu wake.

Unadhani ni kweli Louis Van Gaal alikuwa ni kocha mzuri na mwenye kuupiga mwingi au ganzi za maumivu ya Rooney (kusema ya mayoni pindi akiwa United chini ya Ferguson) ilikuwa imeisha? tujiunge na ripota wetu Ester Maongezi kutoka Sports Bomba ya Plus TV channel namba 294 kwenye king’amuzi cha DStv, Jumatatu hadi Ijumaa 2:30 za usiku kwa taarifa kamili.

Ndugu msomaji unadhani na wewe kwenye eneo lako…………………….anaupiga mwingi kama msemavyo au ganzi ya watu kusema ya moyoni sasa hivi imekwisha? tupate mapumziko mafupi kutoka kwa wahisani wetu DStv channel 294 kisha tutarejea.