Adam Adam uko wapi………………Je, umekula matunda ya mti niliyokukataza?”

Happy Father’s Day

Kwa kosa lako ardhi imelaaniwa, kwa jasho utajipatia humo riziki yako, siku zote za maisha yako mpaka utakaporudi udongoni ulimotwaliwa kwa maana wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi.”

Heri ya siku yenu wakina Baba.

Juni 20 kila mwaka dunia huazimisha siku ya wakina baba ulimwenguni kote kwa minajili ya kuukumbusha uwepo wao, niliwahi kukaa na kujiuliza kwa kina juu ya umuhimu wa siku hii hasa kwa wakina Baba lakini bado sikupata majibu ya kutosha na yenye kueleweka. Kwa tafiti chache zilizopo mwanaume (Baba) amekuwa si mtu kupewa attention kwenye mambo mbalimbali hasa yale ambayo ni chanya ni mara chache mno kukuta Baba akipewa appreciation kubwa ya kuilinda, kuihudumia au hata kuijali familia yake kwa ufasaha ukiachilia mbali kuwa ni majukumu yake tofauti na kwa wenzi wao ambao wao public announcement za appreciation zimekuwa zikijaa mno kwenye nguzo.

Hata ukirudi shuleni, unaweza kuta mtoto wa kiume kalipindua pindua na kuligaragaza vibaya vibaya darasa zima kwenye jaribio fulani lakini kelele za pongezi na mshangao zinakuwa tofauti na endapo jambo hilo jema likafanywa na binti, iko hivyo kiuhalisia tunajua mwanaume ana uwezo na hata ukirudi mwanzo kwenye uumbaji tayari alishavikwa mabomu (kwa lugha ya vijana)
tofauti na mwanamke ambaye mara zote huwa anahitaji kuwaprove watu wrong.

Mwanaume tajiri namba moja duniani, mwanaume Rais wa Taifa fulani duniani, mwanaume mwenye taasisi kubwa za kibiashara, Baba alieilea familia peke yake kwa kipindi chote hadi sasa watoto wake wanajitegemea“………aaanh sawa vizuri

Mwanamke tajiri namba moja duniani, mwanamke Rais wa Taifa fulani duniani, mwanamke mwenye taasisi kubwa za kibiashara, Mama ameilea familia peke yake kwa kipindi chote hadi sasa watoto wake wanajitegemea”……….eeenh Bwana wee, hatari, nani kama mama, noma na nusu, mwanamke shujaa huyu na hata ukilipia kifurushi chako cha DStv Bomba kwa Tsh.19,900 ili utazame Mtazamo ya Plus TV channel namba 294 on DStv kuanzia saa 1 za usiku, utakuta mojawapo kati ya hayo makubwa yaliyofanywa na mwanamke yakizungumziwa kwa kina na Masoud Kipanya & Rahma Mwita tofauti na akifanya Mwanaume/Baba.

“Baba ameitelekeza familia yake, Baba hatimizi majukumu yake ya kimalezi, Baba anamnyanyasa sana Mkewe” hapa ndipo utakagundua kuwa macho yote mawili ya watu huwa kwa Baba, ukifanya chanya watamezea lakini pale unapokosea au kupita njia isiyo sahihi basi watapaza sauti kwa ukubwa ili wakurudishe kwenye mstari jambo ambalo si baya na hii ni kama iliwekwa na Mwenyezi Mungu tangu enzi za uuambaji hivyo ukiwa Baba inabidi ulitambue na ulikubali hili.

Mimi ni nani niache fursa hii kwenye siku yenu kubwa kupiga spana palepale kwenye mshono? huo ndiyo uwanaume/Ubaba ukiona kimya ujue unafanya vizuri lakini ukikosea basi tutasimama kupaza sauti. Baba usifanye majukumu yako kwa lengo la kupata appreciation za moja kwa moja au za wazi wazi fanya majukumu yako kwa ufasaha wake watoto wako wakivaa vizuri, wakiishi vizuri, wakipata elimu nzuri, wakiwa na furaha muda mwingi basi tutakusifu kimoyo moyo na tuta appreciate kuwa unatimiza majukumu yako.

Ukipanga kreti za bia na kutupa ofa, tutakunywa, tutakusifia na tutakuita kila aina ya jina lakini pindi utakaposhindwa kutimiza jukumu lako moja tu kwenye familia tutapaza sauti kwa wingi wake, hata ikitokea mwenza wako akatunza sana nguo au fedha kwenye masherehe ya wengine halafu watoto wako wakakosa nguo ama chakula sisi tutaanza moja kwa moja na wewe kama kichwa cha familia kuwa hautimizi majukumu kwa ufasaha.

Hata ukirudi mwanzo, shetani alimlaghai mwanamke kula tunda la mti uliokatazwa na mwanamke/Mama akala kabla ya kumshawishi mwanaume/Baba naye kula lakini Mwenyezi Mungu alipofika alianza moja kwa moja na kumuhoji Baba/Mwanaume wala si Mwanamke/Mama rejea mwanzo mwa andiko letu.

Vitu vingi vya familia kwenye misingi mizuri vinaanzia kwako Mwanaume/Baba muongoze vizuri mwenzi wako na watoto ili mpite kwenye njia bora, ukiwa hasi ukamuongoza vibaya mwezi wako na watoto basi familia itaenda kupalanganyika.

Heri ya siku ya wakina Baba, tuendelee kukumbushana majukumu yetu ili tusimame kwenye mstari kuepuka kuteleza tusije tukapaziwa sauti. Kwa makosa yako familia yako itapitia wakati mgumu mpaka utakaporudi mavumbini na tabia zako ovu bado utaziacha kama urithi kwa watoto na uzao wako.

Washua wote hongereni kwa kupewa heshima ya appreciation ya angalau kwa siku moja leo, timizeni majukumu yenu kwa ufasaha matokeo yataonekana kwenye familia na uzao wenu.