Ukiwa mkubwa unataka kuwa nani?

Je, unataka kuwa kama Rais wa kwanza mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan?, au unataka kuwa miongoni mwa wenye fedha nyingi nchini ili utokee kwenye orodha ya jarida la Forbes?, ama unataka kuwa kama Bondia Hassan Mwakinyo atakayeongoza listi ya wababe wa kitanzania watakaoshuka ulingoni kwenye mapambano ya #RumbleInDAR usiku wa Mei 28 na kuruka mubashara kupitia king’amuzi cha DStv channel namba 294, Plus TV?

Huenda usiwe na ndoto tena za kuwa kama fulani kwa kuhisi labda umeshapoteza muda lakini una uwezo wa kuwa daraja la vijana wako, ndugu zako au wadogo zako kufikia ndoto ya kuwa kama fulani wakiwa wakubwa. Jiunge na benki ya KCB Tanzania sasa ili uweze kuhifadhi fedha itakayokuwezesha kufanya miamala ya kulipa karo za shule, kufanya manunuzi ya vifaa vya shule na kununua mahitaji mbalimbali kwa urahisi ili vijana wako au wadogo zako waweze kupata fursa nzuri ya walau kwenda kutoa ujinga na kuyavaa maarifa ili wakiwa wakubwa wawe kama…………………baada ya hapo ukae kwa kutulia usubiri matokeo.

Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka mgumu kwa Mfakamia nyavu hatari kutoka viunga vya Santiago Bernabeu pale kwa mzee wa bweta Florentino Perez, mwanaume aliyezitungua nyavu kwa viungo vyake vyote vya mwili, mwanaume aliyewapa jeuri mashabiki wa Real Madrid ya kuamini kuwa wao pekee ndiyo wenye kustahili kuwa na wachezaji bora duniani. Wakati wengi wakiamini kuwa mwanaume huyu ndiyo wakati wake sahihi wa kukiongoza kikosi cha timu yake ya Taifa (Ufaransa) kwenda kwenye kilele cha mafanikio mara baada ya kufanya makubwa ndani ya klabu ya Real Madrid tena akiwa mbichi wa miaka 27 tu, Oktoba 2015 zinatoka taarifa rasmi kutoka kwa shirikisho la soka la Ufaransa kuwa mwanaume huyo ambaye ni Karim Benzema amesimamishwa kuitumikia timu ya taifa hilo ili kupisha uchunguzi wa madai yanayohusiana na kanda chafu ya ngono.

Ipo hivi, ngoja tupitishane kwa uchache kwenye sakata hili la kanda ya ngono ili tusimame kwenye kituo kimoja, Mathieu Valbuena a.k.a Andunje ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa Benzema na mchezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa alipata mlupo wakiwa kwenye harakati zao vijana (kuruka madebe) Valbuena akauchukua ule mlupo wakaingia hoteli wakafanya yao huku wakijirekodi, siku zikapita lakini kwa bahati mbaya ule mkanda ukatua mikononi mwa mahalamia ambao walitishia kuuvujisha mkanda huo endapo wasipopewa fedha za kutosha basi wakashiniķiza kupewa fedha hizo haraka huku wakimtumia zaidi Benzema ambaye alikuwa ni rafiki wa Valbuena kumsisitiza rafikiye atoe fedha hizo.

Karim Benzema na Mathieu Valbuena 

Benzema akawa anamshawishi Valbuena mara kwa mara kutoa kiasi hicho cha pesa ili kuepuka udhalilishaji huo ambao ungemkuta baada ya kuona rafiki yake (Benzema) anamsihi sana kutoa fedha hizo Valbuena akaingiwa na wasiwasi na kuhisi kuwa rafiki yake ni miongoni mwa mahalamia wale hivyo wanampumbaza ili wampige fedha, ikabidi aende Polisi amshushie zigo rafiki yake na hapo ndipo mambo ya Benzema yakaharibika. Benzema akala nyundo ya kusimamishwa kuitwa timu ya Taifa bila matumaini yoyote akiwa kijana mdogo kabisa, unakumbuka kisanga cha Robert Mancini na Carlos Tevez, Mancini na Mario Balotelli je, vipi cha mtukutu Joey Barton baada ya kukosa michezo kadhaa kwenye timu zao?

Basi maisha yakaendelea na Benzema akiwa hajui rangi ya timu ya Taifa lakini hatimaye baada ya miaka takribani 6 Karim Benzema anaitwa tena kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kinachojiandaa na michuano ya Euro 2020 chini ya kocha Didier Deschamps akiwa na umri wa miaka 33.

Licha kutishia mara moja kuhama utaifa baada ya kutokuwa na matumaini yoyote ya kuitwa tena timu ya Taifa ya Ufaransa, Benzema alitulia na akaanza kufanya kazi kweli (kucheza mpira), alizifumania nyavu kadri alivyoweza akiwa na matumaini ya kuitwa tena timu ya taifa siku moja, alibeba vikombe kadri alivyoweza akiwa na matumaini ya kuitwa tena timu ya taifa siku moja.

Ni Benzema huyu huyu aliyoonyesha nidhamu kubwa licha ya kuachwa kwenye kikosi cha Ufaransa cha mwaka 2016 kilichofika fainali ya Euro na kufungwa na Ureno ya kina Cristiano Ronaldo ambapo kwenye mchezo huo ilionyesha wazi kabisa kuwa endapo Ufaransa ingekuwa na mshambuliaji wa kariba yake walikuwa wanabeba ndoo hiyo, hebu niambie mfano wangeachwa Zlatan Ibrahimovic, Diego Costa au Lionel Messi kwenye timu zao za Taifa na zingepoteza fainali wangetoa maneno yenye ujazo gani? lakini haikuwa hivyo kwa Benzema.

Walienda kwenye kombe la dunia 2018 nchini Russia wakiwa na watoto wadogo na wakachukua ubingwa ambao kama Benzema angeitwa hata kwa kukaa Benchi tu angeweka historia ya kushinda Kombe hilo kwa mara ya kwanza na huenda ndiyo ya mwisho kwake lakini wakampiga chini leo wanamuita kwenda Euro? ingekuwa Cristiano Ronaldo unaamini angekubali kweli kwenda pale Ureno kwa staili hii?

Mwanaume anayekiwasha mbele ya Magalacticos pale Santiago Bernabeu ambao karibu wote walikuwa wanaenda timu zao za Taifa kasoro yeye tu kwa miaka 6 mfululizo leo anaitwa timu ya Taifa akiwa anaenda uzeeni, ungekuwa wewe ungekubali?

Mwanaume kapoa kayaacha ya nyuma kaamua kufungua ukurasa mpya haijalishi ameumizwa kiasi gani kwani ny’aaa ya kale hainuki mwanaume ameshukuru na amekubali kwenda kulipigania Taifa lake tena akiwa na umri wa ukingoni kwenye soka.

Ni kipi kikubwa cha kujifunza kwa mwanaume huyu kama siyo kutamani kuwa kama yeye kwenye ukomavu huu mkubwa aliouonyesha? NIKIWA MKUBWA NATAKA KUWA KAMA KARIM BENZEMA.