Baada ya takribani miaka 7 ya innovationweektz mtoto mwingine amezaliwa leo, uzinduzi rasmi wa program mpya ya #funguo ndani ya wiki ya ubunifu tayari umefanyika rasmi kwenye Jengo la Millenium Tower ambapo tukio la Wiki ya ubunifu lilofanyika tarehe 17 May 2021, na kuoneshwa mubashara on DStv channel namba 294, Plus TV.

Hakuna ubunifu bila Afya bora, hakuna uchumi bila Afya bora, kanuni za kujikinga na maambukizi ya Corona zimezingatiwa kwenye tukio la wiki ya ubunifu Tanzania innovationweektz moja kwa moja kutokea Millenium Tower II.

“Tunawashukuru vijana kwa kujitokeza zaidi kusudi tuweze kutembea pamoja kufanikisha hiyo ndoto ya uchumi wa viwanda nchini Tanzania, mpango wa tatu unaongelea ubunifu wa teknolojia kama sehemu ya kuongeza tija kwenye uzalishaji” – Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia costechTANZANIA Dkt. Amos Nungu.