Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea ripoti ya kamati maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona COVID -19 nchini kutoka kwa mwenyekiti wa kamati hiyo Prof. Said Aboud Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

Kamati Maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 17 Mei, 2021 itawasilisha kwa umma taarifa ya Tathmini ya ugonjwa wa Corona (Covid-19).

“Kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini hata hivyo kamati imebaini kuwa muamko wa kudhibiti wimbi la kwanza ulikuwa mkubwa ukilinganisha na wimbi la pili”

“Serikali ihulishe mipango ya dharura katika ngazi zote katika kukabiliana na majanga ikiwemo janga la COVID-19 pia serikali itoe taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua zote za kinga” – Mwenyekiti kamati maalum COVID – Prof. Said Aboud.

“Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa Corona kwa umma na shirika la afya duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka mamlaka za serikali”

“Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa COVID-19 katika kuweka au kutoweka shuruti ya lockdown na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi” – Mwenyekiti kamati maalum COVID – Prof. Said Aboud.