Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani 7, amemuongezea muda Jaji wa Mahakama ya Rufani 1 na ameteua Majaji wa Mahakama Kuu 21.

Katika uteuzi huo aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Eutropius Mgaga na aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Ayoub Yusuf Mwenda wametueliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu.Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa tarehe ya kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu itatangazwa baadae.