Plus Cares kwenye lengo la kurudisha fadhira kwa jamii , imeamua kufturisha watoto yatima kutoka vituo mbalimbali ili kurudisha tabasamu lao kama watoto wengine. sote tunafahamu vyema jamii ya kitanzania, jamii yenye matabaka ya walionacho na wasionacho ambao wana hitaji ya maisha na wala si mali.

Jamii iliyozungukwa na yatima,watoto wa mitaani wajane, walemavu ambao wanatamani kuishi angalau robo ya maisha ambayo unaishi wewe (Mwanafamilia wa Plus).

Wanafamilia wa Plus TV kutoka maeneo mbalimbali ni miongoni mwa watu waliojumuika katika Plus Cares Iftar siku ya jumamosi pale Oasis village club na watoto wetu wenye uhitaji maalum.

Asante kwa kuwa sehemu ya faraja na tumaini jipya kwa watoto wetu wenye uhitaji maalum kwasababu miongoni kwao wapo kwenye ndoto za kuwa warembo wa dunia.