Kuelekea usiku wa Rumble in Dar Second Edition kwa udhamini wa KCB Bank ambapo Mabondia Hassan Mwakinyo JR na Ibrahimu Class watakua wakiiwakilisha Tanzania pamoja na mabondia wengine kutoka nchi mbalimbali kwenye ndondi zitakazopigwa Machi 26, 2021.

Alhamisi hii ya Machi 11, 2021 waandaaji wa mapambano  haya makubwa watazungumza na wanahabari wote nchini kwenye Hoteli ya Onomo iliyopo Posta jijini Dar es Salaam, kuelekea mapambano haya ambayo yatarushwa mubashara kupitia DStv channel namba 294, Plus TV.

Unaweza kutazama mazungumzo haya kati ya waandaaji wa Rumble In Dar Powered by Jackson Group Sports, Global Boxing Stars, KCB Bank, Plus TV, Onomo Hotel, DStv Tanzania na wanahabari wote popote ulipo barani Afrika kupitia kisimbuzi cha DStv channel namba 294, Plus TV Alhamisi hii kuanzia saa 5 kamili za asubuhi.