Ilinichukua miaka kadhaa kidogo kuja kumgundua na kumfahamu mwanzilishi wa miongoni mwa matamasha makubwa ya muziki barani Afrika, tamasha la Sauti za Busara.

Hili ni miongoni mwa matamasha machache barani Afrika yanayoendelea kutunza na kuenzi muziki wenye vionjo na tamaduni halisi za kiafrika kama ilivyokuwa kwenye show ya The Giants ya Plus TV ya Julai 18 ya mwaka 2020 ambapo waliamua kuupa heshima na kuuenzi muziki wa Afrika kwa zaidi ya masaa 3 kwenye episode ya The Giants Sound Of Africa.

Nilitahamaki na kushagaa kwa mara ya kwanza, pale nilipoona mahojiano ya moja kwa moja ya Mgengee kutoka Plus TV na muanzilishi wa tamasha la Sauti za Busara, Mr. Yusuf Mahmoud. Fikra, mawazo, mategemeo na maono niliyokuwa nayo kabla kuhusu tamasha hili na muanzilishi mwenyewe, vilikuwa tofauti na nilivyokuja kukutana navyo, sijui ni kwanini hasa kwa kipindi chote hichi Mr.Yusuph hakupambana kutengeneza jina lake liwe kubwa na maarufu sawa sawa na lilivyo tamasha hilo alilolianzisha.

Utaratibu tuliouzoea sisi ni tutu bene, man to man, chapa iende na jina liende na sivyo hivi tuonavyo kwa Mr.Yusuph na Sauti Za Busara.

Niliwahi kufanya utafiti mdogo wa kuona namna chapa na baadhi ya majina ya watu waliopo kwenye mfumo wa kuziendesha zinavyoenda sambamba, kwa kiasi chake utafiti huu ulitiki lakini pia kwa kiasi chake utafiti huu ulifeli. Leo hii ukitaja jina la Baraka Shelukindo basi MultiChoice Tanzania itakuja usoni kwako, leo hii ukitaja jina la Clouds Media basi Jina la Joseph Kusaga litakuja usoni kwako, leo hii ukitaja Plus TV basi jina la Ramadhan Bukini litakuja usoni mwako, lakini hii haiko hivyo kwenye baadhi ya maeneo.

Ulishawahi kujiuliza muanzilishi wa kampuni inayotengeneza lile gari la ndoto yake ni nani, Je, ana umaarufu sawa na gari yake ilivyo maarufu?

Ulishawahi kujiuliza muanzilishi wa kampuni inayotengeneza simu unayotumia, pikipiki uliyopanda leo, runinga unayotazama kila siku na vitu vingine vingi unavyotumia na kukutana navyo mara kwa mara anafananaje, Je, Jina lake ni kubwa kama ilivyo chapa yake na kuna ulazima wa kukuza jina lake kuwa kama ilivyo chapa yake?

Kwani, tunanua Jina lake au chapa/bidhaa iliyoko sokoni? Nadhani ukipata majibu hapa tutakubaliana kwa pamoja kuwa aendelee tu kubaki la jina lake mfukoni kwani alituhusu sana mradi tunapata bidhaa zake kwenye ubora ule ule ama nini? basi tuendelee

Na hivi ndivyo ilivyo kwa Mr.Yusuph Mahmoud, muanzilishi wa Tamasha la Sauti za Busara ambaye kwa miaka yote amekuwa akipambana kuiweka chapa ya Suati Za Busara mbele zaidi kuliko kitu chochote ikiwemo jina lake na tamasha hili limekuwa likiacha historia na kufanya vizuri kila mwaka pale Visiwani Zanzibar.

Wapo watu wengi ambao wamekuwa wakiota na kutamani kuwa sehemu ya historia ya tamasha hili aidha kwa kushuhudia au kwa wasanii kushiriki kwenye kuperfom katika jukwaa moja ambalo huwa linawakutanisha wasanii maarufu kutoka mataifa mbalimbali.

Huenda wewe pia ukawa ni miongoni mwa wanaotamani kuwa sehemu ya kushuhudia tamasha hili siku moja lakini labda hautaweza kwenda visiwani Zanzibar ambapo tamasha hili linafanyika kutokana na majukumu mbalimbali au changamoto ya kifedha (nauli, malazi, chakula n.k)

Sasa, Plus TV wameliona hilo na inataka kukupitisha moja kwa moja kwenye njia za muanzilishi wa Tamasha la Sauti za Busara, Mr.Yusuph Mahmoud, siyo lazima uwepo wako kimwili uwe Zanzibar bali hapo hapo ulipo kwa gharama ya shilingi 19,900 tu ya kifurushi cha Bomba unaweza kutazama kila kitakachojiri kwenye tamasha la sauti za Busara 2021, tarehe 12 ya mwezi huu wa pili LIVE kupitia DStv channel namba 294 kuanzia saa 3 kamili za usiku.

Hapa utapata kuona hali zote zinazoendelea kwenye tamasha hili kubwa na kuingia kwenye historia ya miongoni mwa waliolishuhudia LIVE ndani ya mwaka huu wa 2021, lipia sasa kifurushi chako cha DStv Bomba ili twende sambamba katika kuandika historia hii kubwa.

Jina lako baki nalo mfukoni, uwepo wako kimwili ubaki hapo hapo Sebuleni kwako lakini Runinga yako itangulize mbele na Plus Television channel namba 294 on DStv uweze kupelekwa moja kwa moja kwenye Tamasha la Sauti za Busara 2021, Zanzibar.