Usiku wa utoaji wa tuzo za The African Entertainment Awards USA (AEAUSA) kwa mara ya sita tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 umekamilika usiku wa jana, Desemba 20, 2020.

Tuzo hizo ambazo zimefanyika nchini Marekani zimeendelea kuwa neema au platform kubwa ambayo wasanii wa Afrika Mashariki wameendelea kuonyesha ubabe wao kwenye kuzitawala katika miaka ya hivi karibuni.

Kwenye utoaji wa tuzo hizo ambazo huwa zinawajumuisha wasanii wote wa Afrika kutoka kwenye mataifa mbalimbali, ukanda wa Afrika Mashariki umejizolea zaidi ya tuzo 8 kupitia wasanii, Djs, watangazaji na wachekeshaji wake.

Diamond Platnumz amefanikiwa kuchukua tuzo kwenye kipengele cha Best Male Artist.Huku The African Princess ‘Nandy’ akichukua tuzo kwenye kipengele cha Best Female Artist.Rayvanny amefanikiwa kuchukua tuzo kwenye kipengele cha Best Male Artist in East/South/North Africa.Wakati tuzo ya Best DJ ikienda kwa DJ Sinyorita.Na Best African Comedian ikienda kwa Eric Omondi wa Kenya.Washindi wengine ni Eddy Kenzo kwenye kipengele cha Entertainer of The Year.Saut Sol kwenye kipengele cha Best Group.Orodha kamili ya washindi wengine wa tuzo hizo.👇