‘Tanzania Stand Up!!, Tasnia ya muziki nchini imeendelea kutakata ndani ya mwaka 2020 kupitia tuzo mbalimbali za kimataifa.

Baada ya Diamond Platnumz, Nandy na Zuchu kufanya vizuri kwenye tuzo AFRIMMA zilizotolewa miezi miwili iliyopita, taa zimeendelea kuwaka kwa wasanii wa kitanzania baada ya kushusha majina manne kwenye tuzo za MTV MAMA ambazo zitafanyika nchini Uganda mwakani.

Wasanii hao ni Diamond Platnumz anayeshindania tuzo katika vipengele vya “Artist of the year” na “Alone Together, Best Lockdown Performance”.

Roma na Stamina (ROSTAM) wanaoshindania tuzo katika kipengele cha ‘Best Group’

Harmonize anayeshindania tuzo katika kipengele cha ‘Best Male’

Na Zuchu anayeshindania tuzo katika kipengele cha ‘Breakthrough Act’.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Februari 20 mwaka 2021, Kampala nchini Uganda.