Mwaka 2020 huenda ukawa wa heshima na mzuri kwa C.E.O wa PKP, Ommy Dimpoz baada ya kupata dili nono la kufanya kazi na Sony Music Entertainment upande wa Afrika.

Ommy Dimpoz, ambaye kwa sasa yupo chini ya Label ya Rockstar Africa, ametoa taarifa hiyo kubwa kuelekea kuufunga mwaka 2020 kupitia ukurasa wake wa instagram.

“Ninayo furaha kujiunga na my new family @sonymusicafrica i can’t wait for my new album to drop early next year” – ameandika Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz anakuwa msanii wa pili kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kufanya kazi na kampuni hiyo kubwa yenye makazi yake Afrika ya Kusini upande wa Afrika baada ya Alikiba.

Sony Music Entertainment imefanya kazi na A-list artists wengi wa dunia wakiwemo, marehemu Michael Jackson, Chris Brown, John Legend, Wizkid, Davido, Mariah Carey na wengine wengi na sasa Ommy Dimpoz anaongezeka kwenye orodha hiyo.