Kilele cha usiku wa tuzo za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) kimefikiwa usiku wa kuamkia leo Novemba 16, 2020 kwa kushuhudia wasanii mbalimbali barani Afrika wakikwarua tuzo hizo kwenye vipengele tofauti tofauti.

Tuzo hizo ambazo tukio lake liliruka live kupitia YouTube channel ya AFRIMMA, limeshuhudia wanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Nandy na Zuchu wakiendelea kung’ara kwa mara nyingine huku wasanii kutoka West Africa wakiendeleza ubabe wao kwenye kuzoa tuzo hizo.

C.E.O wa WCB, Diamond Platnumz alifanikiwa kushinda tuzo kwenye kipengele cha Afrimma Best Male East Africa wakati The African Princess ‘Nandy’ akishinda tuzo kwenye kipengele cha Afrimma Best Female East Africa na Zuchu akikwarua tuzo kwenye kipengele cha Afrimma Best Newcomer.

Wasanii wengine waliofanikiwa kuibuka kidedea kwenye tuzo hizo ni

1.Burna boy kutoka Nigeria kupitia kipengele cha Crossing boundaries with music award,

2.Nasty C kutoka South Afrika kupitia kipengele cha Best Male Rap Act.

3.Mr.Flavour kutoka Nigeria kupitia kipengele cha Best live Act.

4.Master KG kutoka South Africa kupitia vipengele vya Afrimma Artist of The Year, Afrimma Song of The Year & Afrimma Best Male Southern Africa Award.

5.Sho Madjozi kutoka South Afrika kupitia kipengele cha Beat female Southern Africa.

6.Don Jazzy kutoka Nigeria kupitia kipengele cha Afrimma Leadership in Music Award.

7.Simi kutoka Nigeia kupitia kipengele cha Afrimma Best Female West Africa Award.

8.Fally Ipupa kutoka Congo kupitia kipengele cha Afrimma Best Male Central Africa Award.

9.Rema kutoka Nigeria kupitia kipengele cha Afrimma Best Male West Africa Award.