Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametuma salamu zake za pongezi kwa mara kwanza kwa rais mteule wa Marekani, Joe Biden na Makamu wake wa rais Mwanamama Kamala Harris.

Biden kwa sasa ni rais mteule wa Taifa hilo lenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani akiwa anasubiri uapisho wa kuwa rasmi rais wa Taifa hilo mara baada ya kumbwaga mpinzani wake Bwana Donald Trump ambaye alikuwa ni rais wa muhula uliopita.

Kwenye salamu zake za pongezi, Dkt.Magufuli amemuhakikishia Biden kuwa Tanzania itadumisha na kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Marekani kwa sasa.