Baada ya hali ya usalama kuanza kwenda vizuri nchini Nigeria sasa ni muda wa wadau wa muziki nchini humo kupokea mafuriko ya kazi za muziki kutoka kwa A list artists.

Ikiwa ni wiki kadhaa tu tangu Wizkid aachie Album yake mpya ya ‘Made In Lagos’ ambayo inafanya vizuri kwa sasa kwenye chati kubwa za muziki duniani tangu itoke, sasa ni zamu ya super star, Davido kushine kwenye anga la muziki la wanaigeria.

Davido ambaye nyimbo yake ya Holy Ground aliyomshirikisha Nick Minaj ilivuja usiku wa jana, ametoa orodha ya mikwaju yake 17 inayopatikana kwenye album yake mpya ya ‘Bettet Time’ inayotarajiwa kutoka ijumaa hii.

Chris Brown, Sauti Sol, Sho Madjozi, Nick Minaj, Lil Baby, Young Thug, Nas na Ckay ni miongoni mwa majina makubwa yaliyoshirikishwa kwenye album hiyo ambayo kwenye cover yake Davido amemuweka binti yake aliyempata na Mwanadada Chioma, David Ifeanyi Jr.