Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyopo Kaskazini mwa Nchi imetangazwa kuwa hifadhi bora katika bara la Afrika kwa mwaka 2020 kwa kushinda tuzo ya Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani.

Serengeti imeshinda tuzo hiyo kwa kuzishinda hifadhi za Central Kalahali ya Botswana, Etosha ya Namibia, Kidepo Valley ya Uganda, Kruger ya Afrika Kusini na Maasai Mara National Reserve ya nchini Kenya.