Mahakama ya Nairobi imewakuta na hatia washukiwa wawili kati ya watatu waliohusika na  shambulizi la kigaidi la WESTGATE lililotokea miaka saba iliyopita.

Watuhumiwa hao wamehukumiwa kwa kosa la kushirikiana na magaidi waliotenda shambulio hilo mwaka 2013 ambao ni Mohamed Ahmed Abdi na mwenzake Adan Hussein Mustafa wanaodaiwa kushirikiana kutekeleza ugaidi huo pamoja na kusaidia wakati  shambulizi hilo likifanyika.

Mshukiwa mmoja anayefahamika kama Liban Abdullaki ndiye aliyeachiwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha dhidi yake.