Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), jana Septemba 28, 2020 kimefanya mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini na wa kisiasa wa nkoa wa Dar es salaam kujadili nafasi ya mwanamke kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.

Mkutano huo ambao miongoni mwa viongozi wa dini waliofika ni sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, sheikh Alhadj Mussa Salum ambaye yeye ameendelea kusisitiza suala la viongozi wa dini kuepuka kutumika kufanya kampeni za siasa katika misikiti na makanisa ili kuepuka kuhatarisha amani ya Nchi.

Aidha, Sheikh Alhadj Mussa amewataka watu mbalimbali kuwaheshimu wanawake na kuwapa moyo pindi wanapotaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

“Kumdharau mwanamke, kumtukana mwanamke, kumdhalilisha mwanamke ni dhambi kubwa tuwape nafasi za kushiriki kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi”. – alisema Sheikh Alhadj Mussa Salum