Idadi ya wagonjwa wa homa ya Corona jijini Dar es Salaam imepungua na kufikia wagonjwa wanne, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameyasema hayo akiwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Tanga.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kipindi cha Corona kilikuwa kipindi kigumu katika Uwaziri wake lakini anamshukuru Mungu kwa namna Tanzania ilivyofanikiwa kukabiliana na virusi vinavyoisumbua dunia.