Baada ya kukaa miezi kadhaa kifungoni mkongwa wa RnB R.Kelly huenda akapewa dhamana kutokana na kesi yake ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo.

Jaji wa mjini Illnois, Harry D. Leinenweber amelikubali ombi la wanasheria wa msanii huyo juu ya kusikilizwa kwa dhamana ya mteja wao ifikapo March 5, mwaka 2020.

Kama R. Kelly akipatiwa dhamana basi atabaki kwenye kifungo cha ndani huku miguu yake ikifungwa kifaa maalum cha kutoa taarifa endapo ana mpango wowote wa kutoroka.
#PlusXtraUpdates