Huenda 2020 ukawa ni mwaka mzuri kwa ‘The Africans Princess’ Nandy mara baada ya kutangaza kufanya ziara yake ya kimuziki nchini Marekani iitwayo NandyUSATour2020.

Ziara hiyo inatarajiwa kuanza rasmi Mei 22 mwaka huu na kumalizika Juni 20 lakini pia mrembo huyo amewaahidi mashabiki zake kuwa ataachia kazi mpya kabla ya ziara hiyo huku akieleza kuwa atatoa maelekezo zaidi kuhusu ziara yake ya barani Ulaya na Nairobi Kenya.

Nandy anakuwa msanii wa kwanza wa kike wa Kitanzania kufanya Tour nchini Marekani ndani ya mwaka huu.