Baada ya mwanamfalme wa Uingereza Prince Harry na mkewe Meghan Markle kutangaza kujiondoa kwenye familia ya Kifalme (Royal Family), leo limetoka tamko jipya.

Malkia Elizabeth II ameripotiwa kuwapiga marufuku Prince Harry na mkewe Meghan kutumia jina Royal kwenye chapa zao ikiwemo tovuti na mitandao yao ya kijamii.
Kwenye mitandao hiyo, wanatumia jina la “Sussex Royal” pia imearifiwa kuwa Malkia amewanyima hadi mamlaka ya kutumia jina hilo kwenye mikataba mikubwa ya kimataifa.